Habari

Mahakama yaamuru mtoto kumlipa mama yake gharama za malezi

Mahakama ya juu zaidi nchini Taiwan imemuru kuwa mwanamume mmoja amlipe mamake karibu $1m (£710,000)kugharamia malezi na masomo ya kuwa daktari wa meno.

Wazazi nchini humo wamekuwa wakiwashtaki watoto wao ili kupata usaidizi wa kifedha lakini kesi hii nitofauti kwa sababu inahusisha mkataba wa maandishi uliofikiwa kati ya mzazi na mwanawe

Uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini humo uliezea kwamba mama yake anakabiliwa na deni la dola elfu mia sita alilopata akiwalea na kuwasomesha watoto wake wawili tangu kutengana na mumewe.

Alikuwa na wasiwasi kwamba wanawe huenda hawatatimiza wajibu wa kumlinda siku za baadaye, ndiposa akaandikisha mkataba na wanawe wa jinsi watakavyomlipa pesa alizotumia kuwaelimisha na kuwatunza.

Kwa mujibu wa mkataba huo ulioletwa mbele ya mahakama, wanawe wawili, punde tu wanavyohitimu kama madakatari wa meno, walifaa kulipa mama yao asilimia 60 ya mapato yao kila mwezi.

Mwanawe wa pili ana kliniki yake ya meno, na alimuuliza amlipe kulingana na mkataba wao.

Mwanawe naye amesema kwamba wakati alipoingia mkataba huo, alikuwa na miaka ishirini tu, na ni ukiukaji wa haki zake kama binadamu na si halali.

Mahakama ya Juu zaidi ilishikilia msimamo kwamba sheria ya mizozo ya kiraia inakubali mtu kufanya mkataba na kuna kiwango fulani kinachoruhusiwa wakati wa malipo.

Mahakama hiyo pia imesema kwamba makubaliano hayo kati ya mzazi na watoto haitaathiri maisha ya wanawe mwanamke huyo, watamudu, na pia mkataba haujakiuka haki yake kwani alikuwa ametimiza umri wa mtu mzima

Mahakama imeamua kwamba mwanawe ambaye ni dakatari wa meno tangu mwaka wa 2003, atimize matakwa ya mkataba wake na mama yake kwa kumlipa deni ambalo limefika kwa dola milioni moja za Marekani

Katika nchi hiyo ya Taiwan, wazazi wakongwe wana mazoea ya kuwashtaki watoto wao wanapokuwa watu wazima na nia ya kupata msaada.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents