Habari

Majaliwa aahidi kulindwa kwa michango ya waathirika wa tetemeko

Waziri mkuu Kassim Majaliwa, amewahakikishia wote wanaochangia katika mfuko wa maafa kwaajili ya waathirka wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, michango hiyo italindwa na kutumika kwa kazi iliyokusudiwa.

waz

Akizungumza katika hafla ya kupokea misaada mbalimbali iliyotolewa na zaidi ya kampuni 17 za mjini Dar es Salaam kwaajili ya waathirika wa tetemeko hilo, waziri Majaliwa amesema michango hiyo itafanya kazi iliyokusudiwa.

“Naomba nitumie nafasi hii kuendelea kuwatia imani kwamba fedha hii mnayoichanga, yote itakwenda Kagera, kama tulivyowaahidi tutasimamia,” alisema Majaliwa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents