Burudani

Hutoisikia tena kazi ya Avril na Darassa, hii ndio sababu

Hutosikia tena kolabo kati ya msanii wa Kenya, Avril na rapper wa Bongo, Darassa, kwanini? Ngoma hiyo ipo kifungoni, walau kwa mujibu wa maneno ya Darassa mwenyewe.

13712740_1146561518719271_511211886_n
Darassa akiwa kwenye studio za Wanene Entertaiment na engineer wa studio hizo (aliyekaa), Avril na producer Abbah Process

“Hiyo project na Avril, ni moja kati ya project ambazo zipo kifungoni tunasema. Hatuwezi kuirelease sababu hatutaki kuingilia taratibu za watu wala watu waingilie taratibu zetu. Project ya Avril haitatoka sababu tulirekodi kwenye studio ambayo tulikuja kutokea tafrani kidogo ya maelewano,” Darassa alimuambia Natty E wa Jembe FM.

13743508_1176217895783341_1876995824_n
Darassa na Avril wakipongezana kwa kazi nzuri ambayo hata hivyo ipo kifungoni na haiwezi kuja kuuona mwanga wa siku tena

Wimbo huo ulirekodiwa kwenye studio za Wanene Entertainment, wiki 8 zilizopita. Tafrani gani hiyo anayoisema Darassa iliyopelekea kazi yake kutiwa kifunguni? Huenda Hanscana akawa anahusika.

13696566_602908076543220_1886403528_n
Avril akiwa na Hanscana kwenye studio za Wanene. Muongozaji huyo hafanyi tena kazi na kampuni hiyo

Wimbo huo ulirekodiwa wakati Hanscana, swahiba wa Darassa alikuwa bado mfanyakazi wa Wanene Entertainment. Baada ya muongozaji huyo kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo, kazi zake zote alizozifanya mikononi mwao, zilipigwa kufuli – ikiwemo kazi ya mwanae Darassa!

13694764_165168167226998_2060242443_n
Darassa na Avril wakiwa kwenye studio za Wanene Ent

Inasikitisha kwasababu Avril alivutiwa na kazi hiyo. “Class is in session! Really amazing getting a chance to hang out/work with @darassacmg and producer @abbah_process,” aliandika kwenye Instagram.

Darassa anabaki na option nyingine – kumleta tena Avril Bongo, kwenda kwenye studio nyingi na kumalizia walichokianza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents