Habari

Mama aishutumu hospitali ya Temeke kumuibia mtoto

Utata umeibuka baada ya mkazi wa Mbande jijini Dar es Salaam, kuishutumu Hospitali ya Wilaya ya Temeke kumuimbia mtoto mmoja, baada ya kujifungua pacha.

Wakazi wa Kata ya Chamazi mtaa wa Pande, Asma Juma na Mumewe, Amir Pazi wakimfurahia mmoja wa mtoto wao wanayedai alizaliwa mapacha katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es Salaam, mwezi uliyopita na mmoja kupotea katika mazingira yasiyofahamika.

Mwanamke huyo, Asma Juma alisema kabla ya kwenda kupewa rufaa ya kujifungua katika hospitali hiyo, alipima kipimo cha ‘ultrasound’ na kuthibitishiwa kuwa ana mapacha.

Asma alisema awali alikuwa akipata huduma za kliniki katika Zahanati ya Serikali ya Mbande, lakini alikuwa amefanya vipimo vya ‘Ultrasound’ katika Zahanati ya binafsi ya Huruma iliyopo Mbande mara mbili na kuthibitishiwa kuwa ana pacha.

“Wakati napelekwa chumba cha upasuaji nilikuwa sina kichaa cha uzazi, siumwi uchungu, siumwi kichwa, siyo kipofu, siyo kiziwi, nasikia kwa masikio yangu na kumbukumbu zote nimezihifadhi kwenye kichwa changu. Ninachotaka ni mtoto wangu,” alisema Asma.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo alikiri kuwapo kwa tuhuma hizo na kusema tayari zinafanyiwa kazi na uongozi.

Source:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents