Habari

Mambo 10 yaliyotolewa na serikali kwa wabunge leo

Alhamisi hii Mei 24, 2018, Katika kipindi cha maswali na majibu bungeni Jijini Dodoma,wabunge mbalimbali wameuliza maswali na kujibiwa na serikali.

Kila wizara imejibu akiwemo Naibu Waziri TAMISEMI,Joseph Kakunda,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na wengineo :Tazama mambo muhimu kwa ufupi yaliyotolewa na serikali:

#Serikali imeendelea kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatenga 10% ya mapato yake kwa ajili ya Wanaweka, Vijana na Watu Wenye Ulemavu – Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda.

#Katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 56.8 zilitengwa na Halmashauri zote nchini na jumla ya shilingi bilioni 17.5 sawa na 31% zilizotolewa kwa vikundi vya Wanawake na Vijana – Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda.

#Katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 61.6 zilitengwa na hadi kufikia Februari, 2018 jumla ya shilingi bilioni 15.6 sawa na asilimia 27 zilikuwa zimetolewa ambapo jumla ya vikundi 8,672 vya Wanawake na Vijana vilipatiwa mikopo – Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda.

#Katika mwaka wa fedha 2018/2019 shilingi bilioni 53.8 zimetengwa kwa ajili ya mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu katika Halmashauri zote nchini – Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda.

#Serikali itaweka utaratibu katika Sheria ya Fedha (Finance Bill) ya mwaka 2018/2019 utakaohakikisha kwamba halmashauri zote zinatekeleza kikamilifu agizo hilo – Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda.

#Serikali ina mikakati mbalimbali ya kupambana na uvuvi haramu mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika kusimamia na kulinda rasilimali za uvuvi kupitia Halmashauri, Serikali za Vijiji na Vikundi vya Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMUs) – Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

#Kuendelea kutoa elimu kuhusu athari za uvuvi haramu kwa mazingira, jamii na uchumi , kufanya maboresho ya sheria ili kuwa na sheria kali dhidi ya uvuvi haramu hasa uvuvi haramu wa kutumia mabomu/milipuko ikiwa ni pamoja na kuweka kipengele cha kuonesha uvuvi haramu ni uhujumu uchumi – Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

#Kuimarisha mashirikiano ya kikanda na kimataifa kwa kushirikiana na nchi mbalimbali zikiwemo nchi za SADC katika kuzuia uvuvi usioripotiwa  (Illegal, Unregulated and Unreported Fishing – IUU) – Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

#Wizara inahamasisha ufugaji wa samaki ili kupunguza nguvu ya uvuvi kwenye maji ya asili. Naomba waheshimiwa wabunge wote  watusaidie kuwaelimisha wananchi kuachana na vitendo vya uvuvi haramu na kushiriki kilinda rasimali za uvuvi – Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

#Serikali imesema kuwa ajali za barabarani husababishwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni vya kibinadamu kwa 76%, vyanzo kiufundi kwa 16% na vya Kimazingira kwa 8% – Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi – Mwigulu Nchemba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents