Burudani

Man Dojo aeleza nyumba yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya zaidi Tsh. Milioni 150

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Man Dojo amesema nyumba yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 150.

Man Dojo amesema kiasi hicho cha fedha ni makadirio kutokana na mali ambazo zilikuwa katika nyumba hiyo.

“Ile nyumba kwa thamani yake ni zaidi ya Milioni 150, kwa sababu pale nilikuwa na mafremu, nilikuwa na studio, nilikuwa na nyumba yenyewe, mifungo, mabanda ya mifungo, na samani,” Man Dojo ameiambia Clouds TV.

Soma Pia: DC Kinondoni atoa tamko juu ya watu wasiojulikana waliovunja nyumba ya Mandojo

Nyumba ya Man Dojo ilivunjwa na mwishoni mwa March mwaka huu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliingilia kati suala hilo na kueleza waliofanya hivyo kujisalimisha polisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents