Michezo

Manara awatuliza mashabiki wa Simba na Vyombo vya Habari ‘kuweni na subira, watapata tabu sana’

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amevitaka vyombo vya habari na mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kuhusu tetesi za usajili za klabu hiyo zinazosambaa mitandaoni.

Image result for haji manara
Haji Manara

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameandika “Mimi ni msemaji mkubwa na ninasemea klabu kubwa nchini ninapotoa taarifa lazima ziwe zimekamilika 100%. so our fans na media please kuweni na subira..Insha’Allah Alhamisi nitazungumza na press kuelezea yajayo ambayo yanafurahisha mno kikubwa wajue watapata tabu sana“.

Kauli ya Haji Manara imekuja baada ya taarifa za klabu hiyo kuwa imemsaini mshambuliaji wa klabu ya Gor Mahia, Meddie Kagere kwa dau la dola $ 50,000 sawa na tsh milioni 113.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents