Burudani

Mandojo na Domokaya kuvunja ukimya na project mpya mwaka huu

Msanii wa muziki Joseph Francis Michael a.k.a Mandojo amesema anatarajia kuvunja ukimya hivi karibuni baada ya kufanya nyimbo mbili ‘Komaa’ na ‘Sita kwa sita’ pamoja na kuandaa project mpya akiwa na swahiba wake, Domokaya wanaounda kundi lao Wamandavaku.

page

Akizungumza na Bongo5 leo Mandojo amesema tayari ameshaanda nyimbo mbili ambazo amemshirikisha Juma Nature na bado anarekodi yimbo mpya pamoja na za kundi lao.

“Kwasasa wategemee mimi na Juma Nature kwanza,unajua watu wamezoea kusikia sauti zile zile, sasa tukaona tubadilike kidogo ndio maana nimeanza kurekodi na Juma Nature kwanza lakini project za kundi letu nazo zinakuja,” amesema Mandojo. “Nilimtafuta Juma Nature nikamuomba ushauri wa muziki kwasababu yeye ni mkongwe, tukapanga mambo na tayari tumesharekodi nyimbo mbili ‘Komaa’ na ‘Sita kwa sita’ nikiwa na Nature. Kwahiyo bado kazi ya kurekodi inaendelea kuna nyimbo kama tano zinakuja. Zipo ambazo yupo Domokaya na kundi zima ‘Wamandavaku’,” alisema.

“Kweli ukimya ulikuwa mkubwa sana sio kwa mwaka jana tu ni muda mrefu tumekuwa tukipokea taarifa kutoka kwa wadau, mnarudi lini?, ndio maana tukajipanga na kuja bila taarifa kwahiyo mwaka huu wadau na wapenzi wa muziki wetu wakae mkao wa kula,sio wimbo mmoja nyingi zinakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents