HabariSiasa

Marekani ilivyotoa msaada Gaza kwa kutumia Parachuti

Marekani imetoa misaada yake ya kwanza Gaza, huku zaidi ya milo 30,000 ikirushwa na ndege tatu za kijeshi. Kanda za video zinaonyesha msaada ukitua kwa parashuti Rafah, mji wa kusini kabisa wa Gaza ambapo karibu Wapalestina milioni 1.5 wamepewa hifadhi.

Operesheni hiyo ilifanywa kwa kushirikiana na jeshi la anga la Jordan, Kamandi Kuu ya Marekani ilisema. Mashirika ya misaada yamesema kuwa kurusha misaada kwa ndege ni njia isiyofaa ya kutoa misaada.

Mkazi wa Gaza aliyekimbia makazi yake Medhat Taher aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba njia kama hiyo haitoshi. “Hii itatosha kwa shule? Je, hii inatosha watu 10,000?” alisema. “Ni bora kutuma msaada kupitia vivuko na bora kuliko kudondosha misaada angani kwa njia ya miamvuli.”

Bofya hapa chini kutazama zaidi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents