HabariSiasa

Marekani inajitolea Afrika kwa hali na mali- Biden

Rais Joe Biden wa Marekani amesema nchi yake inajitolea kwa hali na mali kwa ajili ya bara la Afrika.

Biden ameyasema hayo kwenye mkutano wa kilele wa siku tatu kati ya Marekani na Afrika mjini Washington.

Mkutano huo ulioanza Jumanne, unahudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa mataifa 49 ya Afrika.

Utawala wa Biden umetowa dola bilioni 55 kuiunga mkono Afrika katika masuala ya ubia wa biashara, usalama wa chakula na mapambano ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hapo jana, Biden alisema tangazo hilo lilikuwa ni mwanzo tu wa mengi mengineyo yanayokuja.

Akiwa mjini Washington, Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema Afrika haipaswi kupuuzwa na haitakiwi kuonekana tu kama sehemu yenye matatizo.

Kagame amebaini kwamba taifa lake na mataifa mengine ya Afrika yatajaribu kuepuka “kuchagua kati ya Marekani na China ambazo zinapambana ili kupata ushawishi barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents