Habari

Mariah Carey na Nicki Minaj wazinguana tena, kidogo wazichape

Nicki Minaj

Ule usemi kwamba mafahari wawili hawakai zizi moja umeendelea kudhihirika kwenye meza ya majaji wa American Idol baada ya Nicki Minaj na Mariah Carey kuzinguana tena.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya nini kilichotokea lakini kuna video inayoonesha Minaj alivyomwakia Mariah.

“If you’ve got a f–king problem, handle it!” Minaj, anasikika kwenye video hiyo akimwambia Mariah kwenye usaili wa jana huko Charlotte, N.C.

Mariah Carey

Mtandao wa TMZ, umedai kuwa Minaj alimtishia Mariah kumpa kichapo!!

Chanzo kimoja cha Idol kimeimba E! News, “This is the sort of thing producers considered might happen when they cast Nikki opposite Mariah, but not this bad and not this fast. They have to protect Mariah to make sure she doesn’t walk. After everything it took to get that panel in place, they need everyone, especially Mariah. She was their first choice.”

Mchana wa jana Mariah alitweet “whyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy,” tweet ambayo hata hivyo alikuja kuifuta baadaye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents