Burudani

Masanja kuja na ‘Street Gospel Ministry’ kusambaza injili kwa Bodaboda au Bajaj

Mchekeshaji Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji ambaye kwa sasa ni mchungaji amekuja na aina mpya ya kuhubiri ‘Street Gospel Ministry’ambapo atakuwa akipita mtaani kwa bodaboda au bajaj.

masanjawani

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Masanja amesema pamoja na kuwepo makanisa mengi kama vile vibanda vya mitandao ya simu kwaajili ya kutolea fedha lakini mwito bado hauridhishi.

“Ninapowaambia watu nimeokoka, wanaziangalia nywele zangu au viatu vyangu, lakini wamesahau Samson alikuwa vipi? Sasa nakuja na Street Gospel Ministry nitahubiri mtaa kwa mtaa iwe kwa bajaji au bodaboda,” alisema Masanja.

Pia amsema atawafuata kondoo popote pale walipo ili kuwachunga na mahubiri yake atayarekodi kisha kuyatengenezea video kwa ajili ya kuwapatia wale wanaotingwa na mambo ya kidunia ili wapate kumjua Mungu. “Siku hizi makanisa ni mengi kama vibanda vya M-Pesa na Tigo Pesa au Airtel Money lakini watu wamekuwa wagumu kumwabudu Mungu sasa nawaletea huduma walipo,” anasema Masanja.

Source: Mwanaspoti

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents