Burudani

Master J: Sio haki msanii kurekodi wimbo kwa laki 2 na kushoot video South kwa milioni 25

Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Master J amekuwa mstari wa mbele kupaza sauti kuhusiana na kutokuwepo kwa usawa kati ya watayarishaji wa muziki na wasanii nchini.

Shaa Master J & Madam Rita

Master J ameiambia Bongo5 kuwa kuna watayarishaji ameshaona wanakosa moyo wa kufanya kazi kutokana hali hiyo.

“Tanzania maprodyuza ni maskini, eti wasanii wana hela kuliko producers hii ni industry gani,” amehoji Master J. “Kwa sababu hapa hizi sheria zilizopo hazimlindi producer ndo maana anadharaulika. Huyo huyo msanii yupo tayari akulipe laki mbili umtengenezee wimbo halafu anauchukua huo wimbo kwenda kutengeneza video kwa milioni 25 yaani wewe acha tu, hiyo ni dharau kubwa sana,” ameongeza.

“Yaani mimi nikiangalia industry nacheka tu, ni matusi. Huyo huyo producer unaweza ukamlipa milioni ukishamlipa milioni asikusumbue tena kwenye revenue share. Yaani unashindwa kumthamini producer hata umlipe milioni kwa sababu ile laki mbili unayolipia ni studio time lakini haujanunua haki yangu. Mimi naona pale wewe sasa hivi huangalii hata Marco ameacha kufanya kazi unafikiria kwanini?

“Amevunjika moyo yaAni moyo wake umevunjika kabisa kwa sababu anaonyeshwa laki mbili halafu huyo huyo anayeonyesha lakini mbili anaenda South Afrika anashoot video ya dola elfu kumi na tano, bila beat huo wimbo wake utaenda wapi? Bila beat wimbo wako utapigwa r
redioni? Unajua maproducer itafika sehemu watachoka kwa sababu sasa hivi wengi wameshaanza kuona dharau, kishingo upande wanalalamika.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents