HabariMichezo

Mayele kama ataondoka Yanga, mimi pia nitaondoka- CEO Senzo akanusha kusajiliwa Kaizer 

Mapema asubuhi ya leo kumeibuka tetesi za Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele kuhusishwa kutimkia Kaizer Chiefs Football Club ya Afrika Kusini.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Mwandishi wa Habari, Nuhu Adams @nuhuadams_ ameandika kuhusiana na sajili hiyo ya Mayele ambayo imezua gumzo mitandaoni.

”South African giants Kaizer Chiefs have completed the signing of Yanga SC striker Fiston Kalala Mayele (28) on a three-year contract, announcement soon. Mayele was 2nd highest scorer in the Tanzania Premier League this season with 16 goals.” ameandika Nuhu.

Baada ya kuibuka kwa tetesi hizo CEO wa Klabu ya Yanga, Senzo Mazingiza amekanusha kwa nyota wao kusajiliwa Afrika Kusini kupitia twitter.

”They must have done a serious magic to sign him while he is still contracted at @yangasc1935,”- Senzo

Kupitia EFM, Senzo amesema kama Mshambuliaji huyo ataondoka Yanga na yeye ataondoka huku akikanusha vikali taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa na Klabu zote mbili Kaizer na Yanga.

”Mayele haondoki Yanga SC na kama ataondoka mimi pia nitaondoka Yanga.”- Senzo alipozungumza na EFM Radio.

Imeandikwa na @fumo255

 

Related Articles

Back to top button