Habari

Mbunge wa CCM aliyedaiwa kupokea mishahara hewa akanusha taarifa hizo

Baada ya kuenea kwa taarifa za Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano huku akiwa tayari ameshaachana na kazi hiyo – mwenyewe amefafanua juu ya taarifa hizo.

prof-normansigalla

Profesa Sigalla alitoa maelezo hayo jana alipofika ofisi za gazeti la Mwananchi ambao ndiyo walitoa taarifa hizo hapo awali za Mbunge huyo kupokea mishahara hewa.

Mbunge huyo amekanusha kiasi cha fedha kilichoingia kwenye akaunti yake kwamba si shilingi milioni 23 kama baadhi ya taarifa zinavyodai bali ni shilingi milioni 5,091,734.96 ndizo zilizoingizwa kwenye akaunti yake ya benki.

Profesa Sigalla amedai kuwa hali hiyo ilitokana na makosa ya ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara kimakosa jambo ambalo alilitolea taarifa mapema kabla hata vyombo vya habari havijaipata taarifa hiyo.

Hata hivyo Mbunge huyo amekiambia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV kuwa kwa sasa hali ni shwari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents