BurudaniDiamond Platnumz

Mchambuzi huyu anaamini ni ndoto Rich Mavoko kusainiwa WCB, hizi ni sababu zake

Mbuke Rashidi aka Mbuke Mchambuzi anajielezea kama ‘ni mdau mkubwa wa social media, entertainment industry pamoja na sports.’ Ametutumia uchambuzi huu kuhusiana na ugumu kwa Rich Mavoko kusaini na label ya Wasafi. Ifuatilie:

Mavoko

Wasafi Classic Baby ama (WCB) kama inavyofahamika na wadau wengi wa burudani ni record label ambayo iliasisiwa na gwiji wa muziki nchini Tanzania Nasibu Abdul(Diamond Platnumz)kama anavyopenda aitwe na mashabiki wake ikisimamiwa kwa karibu na wanaoaminika kuwa ni wasimamizi bora kabisa wa kazi za muziki wa kizazi kipya kwa sasa nchini Tanzania ambao ni Babu Tale,Mkubwa Fella pamoja na Sallam SK.

Kwa kiasi kikubwa label hii imefanikiwa kupush sanaa ya Tanzania na kuipeleka mbele zaidi sio tu kwa upande wa waimbaji bali hata dancers,wapiga picha pamoja na producers.

Ukimuondoa Diamond Platnumz ambaye ni boss, currently record label hii ina wanamuziki wawili ambao ni Harmonize kijana kutoka kijiji cha Chitoholi wilayani Tandahimba mkoani Mtwara anayefanya poa na hit song yake aliyomshirikisha bosi wake (Bado)pamoja na kijana mwingine aitwaje Raymond(Rayvanny) ambaye kiasili ni mwenyeji wa mkoa wa Mbeya anayesumbua pia mtaani na ngoma yake (Kwetu) iliyomtambulisha rasmi katika industry hii

Lakini kwa siku za hivi karibuni kupitia media mbalimbali kumekuwepo na tetesi ambazo zinamhusisha msanii A list katika kiwanda cha Bongo Flava, Rich Mavoko kuwa signed katika label hii.
Rumors ambazo ziliasisiwa na boss wa label hii Diamond Platnumz alipofanya mahojiano na (AYOTV) na kueleza kuwa Mavoko alitakiwa awe signed na Wasafi kabla hajatoa hii ngoma yake mpya(Naimani)

“Ilitakiwa itoke under management ya Wasafi lakini kuna vitu vilichelewesha deal hiyo,” alisema Diamond.

Tetesi hii baadaye ilikuja kuongezwa nguvu na Harmonize mmoja wa wasanii walio chini Wasafi pale alipothibitisha kuwa Wasafi ina wasanii watatu ambao wako signed akiwemo yeye mwenyewe,Raymond pamoja na Rich Mavoko, tetesi ambayo baadaye ilikuja kukanushwa na Sallam, meneja wa Diamond pamoja na Rich Mavoko mwenyewe

Licha ya kuwepo na ukweli juu ya mazungumzo yaliyofanywa kati ya management ya wasafi pamoja na Rich Mavoko, bado mimi sitaki kuamini kukubali kuwa Mavoko anaweza kweli comfortably kuwa under Wasafi management inayoongozwa na Diamond ingawa hakuna shaka kuwa deal hii inaweza kuwa ni yenye tija kwa wote wawili kutokana na resources ambazo wawili hawa wanazo.

Tukumbuke kuwa Diamond ana connection kubwa ya nje pamoja na fund ya kuinvest kwa Mavoko huku Mavoko yeye akiwa na talent kubwa ya uimbaji pamoja na utunzi usio na shaka lakini bado ninapata mashaka makubwa na imani yangu inanifanya nijiridhishe kuwa hii deal haiwezi kukamilika kutoka na makandokando haya:

1. NAFASI YA RICH MAVOKO KATIKA MUZIKI WA BONGO FLAVA

Hapana shaka kuwa Rich Mavoko ni miongoni mwa A list katika wasanii wa Bongo Flava na anayo fan base yake ambayo pia ni kubwa ingawa hana mafanikio ya kutisha sana katika industry hii.

Kuna time ambayo Rich alikuwa nyuma ya Diamond akiwa kama mshindani wake mkuu kutokana na style ya muziki wao hali iliyokua inapelekea kutokea kwa misunderstanding za mara kwa mara kati yao hadi kutuhumiana uchawi. Sasa basi Mavoko kwenda kusign katika label iliyo chini ya aliyepata kuwa hasimu wake ambaye anaamini ana kipaji kikubwa pia ni kama ”Kujishusha”na “Kujidhalilisha”ingawa kwa sasa ukweli ni kwamba hawa watu hawako tena katika level zinazofanana.

2.UWEPO WA BABU TALE NA MKUBWA FELLA

Hakuna ubishi kuwa kwa kiasi kikubwa muziki wa Bongo Flava umeshikiliwa mikononi mwa hawa jamaa wawili. Wanaaminika kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuwa na uwezo wa kusema huyu “AWE huyu ASIWE” na mara nyingi wamekua wakigubikwa na shutuma mbalimbali kutoka kwa wasanii kama “Unyonyaji” na shutuma nyingine nyingi ingawa pia tunafahamu hakuna binadamu mkamilifu.

Watu hawa wanapenda kuheshimiwa kwa kiasi kikubwa na mara nyingi hupima nidhamu ya msanii kwa kumpa msoto sanaa rejea kwa Raymond na wengine msoto ambao unahitaji uvumilivu na busara ya hali ya juu kuweza kuuvuka kitu ambacho kwa hulka na tabia ya Mavoko hawezi kukivumilia na kuna uwezekano mkubwa wa kupishana Kiswahili na hawa watu wawili na kwa kulitambua hili ninaamini hii ni miongoni mwa sababu zinazofanya deal ya Mavoko na Wasafi kuwa ngumu zaidi.

3.KUKOSA UHURU WA KUFANYA MAMBO BINAFSI KWA WAKATI

Labda niseme tu kuwa Rich hajaishi na kukulia katika maisha au mazingira yanayomuhitaji kufuata utaratibu zaidi kama ambavyo wasanii walio chini ya label ya Wasafi wanavyoishi.Inasemekana ukiwa Wasafi ni kazi nonstop haina ile kuhang kwenye viwanja vya starehe kama vile clubs na maeneo yanafanana na hayo mara kwa mara na muda mwingi wanautumia wakiwa ndani(studio) wakirekodi ngoma au kufanya mazoezi. Kifupi maisha ya wasafi ni kama academy.

Kwa wasanii wachanga na wanaotafuta tobo kama Harmonize na Raymond hii inaweza isiwe kazi ngumu kwao hata kidogo lakini kwa msanii mkubwa wa aina ya Mavoko lazima kutakua na ugumu fulani kwakuwa anaweza kukosa ule uhuru wake wa mwanzoni wa kuhang na washkaji au kupata time ya kufurahi na baby wake na vitu kama hivyo

4. DIAMOND PLATNUMZ MWENYEWE

Siamini kama kuna kitu kigumu kama kumsimamia mtu mliye katika industry moja mfano muimbaji kumsimamia muimbaji mwenzake na hasa ikiwa huyo muimbaji (msimamiaji)bado anafanya muziki wa ushindani.
Hapa kuna mambo yanaweza kutokea msimamiwaji kushindwa kupiga hatua,msimamiaji kushuka thamani yake(kimuziki)au wote kushindwa kuendelea.
Imagine Diamond na Mavoko wote wanawania tuzo lets say wimbo bora wa mwaka au msanii bora wa kiume na Mavoko akabeba hiyo tuzo ushajiuliza au kufikiria ni nini kinaweza kutokea?

Inaweza isiwe shida kubwa kwa wenzetu ambao wametutangulia na kuwa na exposure kubwa lakini haiwezi kuwa rahisi kwetu sisi ambao hatuna ukomavu na kisanaa(boss kwanza wengine wanafuata).Rejea ugomvi wa Bob Junior na Diamond Platnumz.
5.DONGO LA RICH MAVOKO KWA HARMONIZE

Wakati Harmonize alipoupa nguvu uvumi wa Rich Mavoko kusign Wasafi, Mavoko alionekana kama kumjibu Harmonize kwa njia ambayo sio rahisi kuigundua pale alipotumia page yake ya Instagram kupost maneno haya, “Ukipata nafasi ya kuongea ongea vya maana ukiongea visivyo na maana utaonekana hauna maana,”ambayo yanaashiria kuwa ni dongo la moja kwa moja kwenda kwa Harmonize ambaye ni wazi anaonekana kuwa msanii kipenzi wa Diamond.

Ni wazi kuwa vijembe kejeli na majivuno ya Mavoko ni vitu ambavyo vinanifanya niamini kuwa deal yake na Wasafi haiwezi kutokea. You can prove me wrong baadaye kama ikitokea lakini kwa sasa msimamo wa kichwa changu ni huu.

Contact: +255 658 019 109 au +255 622 019 109
Mail: [email protected]
Facebook:Mbuke Mchambuzi
Twitter: @VocalYaJesus
Instagram: @Mbuke_themanini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents