Picha

MeTL Group yazindua kampeni ya ‘Usikate Tamaa’

Kwa kutambua hali ambayo inawakuta watu wengi katika jamii na kupoteza matumaini ya kufanikiwa kimaisha, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.

907b8cea-f7f9-4cdb-82fd-056664bd9e6f

Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.

2ecaa60a-730a-4d13-a217-d79bbebb5373
Meneja Masomo wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Fatema Dewji akizungumza na waandishi wa habari Jumanne hii

Alisema kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali na sasa wamefanikiwa kimaisha.

“Kuna watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.

Maneja masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.

“MeTL kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu zaidi,” alisema Fatema.

Kwa upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.

4b856fa6-1b23-42e3-bd84-c6d4cfbea684

“Unaweza kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi nifanye hivyo,

“Ilikuwa naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents