Meya Sitta atangaza neema kwa wavuvi Kinondoni (Video)
Meya wa Manispaa wa Kinondoni Mh.Benjamin Sitta amezindua rasmi maadhimisho ya siku ya wavuvi dunian ambapo amewaasa wavuvi hao kuepuka uvuvi haramu.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika soko la samaki Msasani wilayani humo ambapo kilele chake kitaifa itafanyika Jijini mwanza hapo kesho.
Meya wa Halmshauri ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza na Wavuvi na wafanyabiashara wa samaki katika soko la Samaki Msasani,Leo wakati wa uzinduzi wa siku ya wavuvi duniani |
Katika hotuba yake sita amewataka wavuvi kuwafichua watu wanaojihusisha na uvuvi haramu hasa wanao tumia mabomu na baruti badala yake watumie uvuvi wenye tija.
Amesema serikali ya manispaa na mkoa wanakuja na mkakati kabambe wa kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa bahari ya hindi.
Afisa Uvuvi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza kwenye tukio hilo. |
Lakin amesema manispaa yake inamkakati mzuri wakuboresha miundombinu ya soko la samaki msasani ili liwe na hadhi ya kimataifa ambapo itaongeza kipato kwa wavuvi na wauzaji wa samaki.
Nae afisa wa Manispaa Bi Grace Kakama Amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na wavuvi katika kuhakikisha wanalinda Rasilimali za uvuvi zilizopo katika ukanda huo wa kinondoni.