Michezo

Mfahamu mchezaji mrefu zaidi katika ligi ya ‘basketball’ ya NBA, akitokea Afrika

Inafahamika kuwa miongoni mwa michezo inayoongoza kuwa na wachezaji warefu duniani ni pamoja na Mpira wa Kikapu maarufu kama ‘basketball’

Image result for Tacko Fall

Taifa la Marekani ndilo linalosifika zaidi kwa mchezo huo, hasa kupitia ligi yake pendwa ya NBA ambayo kirefu chake ni ‘National Basketball Association’.

Tacko Fall, kwa sasa anatajwa kuwa ndiyo mchezaji mrefu zaidi kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya NBA nchini Marekani.

Tacko Fall mwenye urefu wa futi  7 na inch 5 ameanza kucheza mpira wa kikapu ‘basketball’ miaka sita (6) iliyopita  huku akivunja rekodi mbalimbali mpaka sasa.

“Mimi bado ni kijana mdogo ninayetokea Senegal, nilianza kucheza mpira wa kikapu ‘basketball’ miaka sita (6) iliyopita.” Tacko Fall ameiyambia BBC Sport Africa.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, mzaliwa wa Dakar nchini Senegal amesajiliwa na timu ya Boston Celtics kwaajili ya msimu wa NBA mwaka 2019/2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents