Habari

Mfanyakazi wa ndani amfunga Waziri wa zamani wa Burundi na Mkewe na faini juu

Mahakama ya jinai ya Nanterre nchini Ufaransa imemhukumu waziri wa zamani wa Burundi na mkewe kifungo cha miaka miwili jela na faini ya euro 70.000 kwa malipo ya uharibifu kutokana na kumtumia mfanyakazi wa ndani kwa kipindi cha miaka kumi nyumbani kwao, Ville-d’Avray, (Hauts-de-Seine).

Image result for Gabriel Mpozagara and Wife

Gabriel Mpozagara, waziri wa zamani wa haki na Uchumi nchini Burundi, na mkewe Candide Mpozagara, wamekutwa na hatia ya kumpa kazi kwa kulazimisha, mfanyakazi huyo, na kumuweka katika mazingira yasiyokuwa ya heshima.

Methode Sindayigaya, mkulima wa zamani wa Burundi mwenye umri wa miaka 39, aliiambia mahakama jinsi alivyokuwa “mtumwa” wa miaka 10 nyumbani kwa wanandoa hao.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Radio France Internationale, Wawili hao wanashtumiwa usafirishaji haramu wa binadamu. Ofisi ya mashitaka jijini Nanterre inawashtumu wawili hao kumnyanyasa raia huyo wa Burundi kwa miaka kumi kwenye makaazi yao, magharibi mwa Paris.

Methode Sindayigaya ambaye alifanyiwa madhila hayo, aliingia nchini Ufaransa akiandamana na mwanawe, huku akibaini kwamba alijaribu kuwaambia wanandoa hao kuwa alipoteza pasipoti yake. Awali Gabriel Mpozagara na mkewe walisema kuwa hawakutaka kumuachilia aende hovyo mitaani. Alikuwa kama “mtoto wa nyumbani, rafiki ambaye wakati mwingine alisaidia na kazi za nyumbani”. Alitaka kubaki katika makazi yangu, alisema Gabriel Mpozagara.

Kwa kujitetea mahakamani Methode Sindayigaya ameileza mahakama jinsi, alitumiwa kuhudumia watoto kwa miezi mitatu. Miaka kumi alifanya kazi saa 19 kati ya 24 huku akilishwa vibaya, makazi duni, na kadhalika, wanasheria wake walisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents