Habari

RIPOTI: Haya ndio majiji 10 tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka 2019, Afrika Mashariki imeingiza Jiji moja tu ‘Dar yapanda nafasi mbili’

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na taasisi ya AfrAsia Africa Wealth Report 2019, Imeyataja majiji 10 tajiri zaidi barani Afrika.

Lagos, Nigeria

Kwenye orodha hiyo ambayo imetawaliwa na majiji mengi kutoka Afrika Kusini, Imelitaja Jiji la Nairobi, Kenya kuwa Jiji pekee kutoka Afrika Mashariki kuingia kwenye 10 bora, Ambalo utajiri wake umekadiriwa kuwa  USD Bilioni  49 sawa na Tsh.  Trilioni 112.7 .

Kwa upande wa Tanzania, Jiji la Dar Es Salaam limepanda kutoka nafasi ya 14 mwaka jana hadi nafasi ya 12 mwaka 2019 likiwa na utajiri wa Dola Bilioni 24 ambazo ni sawa na Tsh. Trilioni 55.

Kwenye ripoti hiyo, Afrika Kusini imeingiza majiji manne ambayo ni Johannesburg (USD Bil. 248), Cape Town (USD Bil. 134) na Durban & Umhlanga (USD Bil. 54) na Pretoria (USD Bil. 45).

Utafiti huo, Umeangalia zaidi biashara zinazofanyika kwenye Jiji husika, Kipato kwa kila mtu na ajira. Jiji la Nairobi ambalo limeshika nafasi ya 6 limetajwa kama Jiji linalokuwa kwa kasi kiuchumi na linatarajiwa mwakani kuingia kwenye 5 bora na kuchukua nafasi ya Jiji la Lagos endapo uchumi  wa Nigeria utaendelea kudhorota.

Kwenye ripoti hiyo Lagos utajiri wake ni USD Bil. 96 wakati Nairobi utajiri wake unakadiriwa kuwa ni USD Bil. 49.Tazama orodha kamili hapa chini. Viwango vya fedha vipo kwenye Tsh.

1. Johannesburg, Afrika Kusini  -Tsh.  Trilioni 570.4

2. Cape Town, Afrika Kusini – Tsh. Trilioni 305.9

3. Cairo, Misri – Tsh. Trilioni 296.7

4. Lagos, Nigeria – Tsh. Trilioni 220.8

5. Durban, Afrika Kusini – Tsh. Trilioni 124.2

6. Nairobi, Kenya – Tsh. Trilioni 112.7

7.Pretoria, Afrika Kusini – Tsh. Trilioni 103

8.Luanda, Angola – Tsh. Trilioni 96

9.Casablanca, Morocco – Tsh. Trilioni 89

10. Accra, Ghana – Tsh. Trilioni 80

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents