Habari

Mganga wa kienyeji kortini kwa kujifanya mwanajeshi

Mganga wa kienyeji mkazi wa Wilaya ya Mpanda, mkoani Rukwa, Majaliwa Rashid (26) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya mkoa, kwa kosa la kujifanya ofisa wa Jeshi la Polisi.

Na Fitina Haule, PST, Morogoro

 

 

 
Mganga wa kienyeji mkazi wa Wilaya ya Mpanda, mkoani Rukwa, Majaliwa Rashid (26) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya mkoa, kwa kosa la kujifanya ofisa wa Jeshi la Polisi.

 

 

 

Ilidaiwa mahakamani hapo jana na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Bw. Salehe Kalulu mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Bi. Emily Mwambapa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 11, mwaka huu saa 3:00 usiku maeneo ya Msamvu katika nyumba moja ya kulala wageni.

 

 

 

Mwendesha Mashtaka alidai kuwa mshtakiwa alijifanya kuwa ofisa wa jeshi hilo kwa wapangaji wenzake waliokuwa ndani ya nyumba ya kulala wageni na kuanza kuwafanyia upekuzi mmoja baada ya mwingine kwa lengo la kujipatia fedha.

 

 

 

Alidai wakati mshtakiwa akiendelea na zoezi hilo, wapangaji wenzake walimshitukia na ndipo wakachukua uamuzi wa kutoa taarifa kwa askari waliokuwa doria katika maeneo hayo na mshtakiwa kukamatwa.

 

 

 

Alidai kuwa baada ya askari hao kumkamata mshtakiwa, walimhoji na baadaye alikiri kuwa hakuwa polisi ila alikuwa anawatisha wenzake ili aweze kupata fedha kwa ajili ya nauli ya kurudia kwao.

 

 

 

Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake alikana na alirudishwa rumande kwa kukosa wadhamini. Kesi itatajwa tena Februari 29 mwaka huu.

 

 

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents