Habari

Mh. Lissu atamani kurudi bungeni ‘Unamkaba Waziri hadi anakosa pakukimbilia’

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa anapenda kazi ya ubunge kwasababu ya mapambano ya kisiasa na kiitikadi ndani ya Bunge huku akieleza kuwa una mkaba Waziri mpaka anashindwa kwa kukimbilia.

Lissu akiongea na Azam News amesema kuwa kuna watu wanapenda ubunge kwasababu unapesa au kutokaa foleni.

“Mimi napenda kazi ya ubunge, kuna watu wanapenda ubunge kwasababu una pesa una manufaa unaitwa muheshimiwa hukai kwenye foleni kwanza hukai kwenye foleni mimi napenda ubunge mule ndani ya hasa yale mapambano ya kiitikadi, na kisiasa mule ndani ya bunge, unamkaba waziri mpaka anakosa pakukimbilia, hiyo ndiyo kazi naipenda mimi, hivyo hakuna kazi ninayoimisi mimi kama kazi ya ubunge bungeni,”amesema Tundu Lissu.

Mbunge Lissu alishambuliwa kwa kupigwa risasi eneo la ‘area D’ mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents