Mbunge wa Makete Mh: Festo Richard Sanga @festosangatz akichangia hoja ya Kamati ya huduma za jamii, Elimu na Michezo amepaza sauti kwa serikali kuongeza kasi swala la ujenzi wa Viwanja vya michezo nchini.
Sanga amesisitiza mapato yanatotokana na Sportbetting (bodi ya kubashiri) yaelekezwe kwenye michezo kwa miaka mitatu mfululizo angalau kwa asilimia 60% ili kuweka mazingira mazuri ya kuandaa miundombinu na timu ya Taifa kwaaajili ya AFCON 2027 hapa nchini.