Burudani

Mike Tee: Ni kawaida wasanii kupokezana vijiti sio kila siku uko wewe tu unasikika

Mike Tee ni miongoni mwa majina ambayo yalivuma kwenye muziki wa Bongo miaka kadhaa iliyopita, kabla hajakabidhi vijiti kwa vipaji vipya kama ambavyo amekiri mwenyewe kuwa ni jambo la kawaida kwenye muziki.

Mike

Rapper huyo kutoka Iringa amezungumzia swala la wasanii wengi kupotea kwenye game na kusema kuwa, ni jambo la kawaida kwa msanii kuvuma na baadae kupotea kwasababu biashara ya muziki ni sawa na biashara nyingine yoyote ambayo kuna wakati inaweza kushamiri na baadae kunyauka.

“Wengi wameshindwa kuhimili ushindani ambao upo, yaani hicho ni kikubwa sana halafu cha pili muziki ni sawa na biashara nyingine zozote sasa kuna kipindi unapata kuna kipindi haupati kitu yaani inategemeana na kazi uliyofanya,” Alisema Myalu kupitia E-Newz ya EATV.

“Sasa wengi unakuta hawana ile plan b, kwa maana ipi, wengi unakuta ule msingi kabla hajaanza muziki alikuwa anafanya nini, amesoma shule amefanya nini, kwahiyo kuna vitu ambavyo ukifeli biashara moja je unakimbilia wapi. Sasa unakuta wengi wanashindwa kuhandle competition ambayo inakuwepo kwanza ya yeye mwenyewe na mazingira alipo halafu cha pili mabadiliko ya muziki, wawe wanaangalia hata kwa nje iko hivyo watu wanapokezana vijiti sio kila siku uko wewe tu unasikika.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents