Tragedy

Video: Magaidi walioshambulia ofisi ya jarida la Ufaransa na kuua watu 12 ni mtu na mdogo wake!

Polisi nchini Ufaransa wamewataja mtu na kaka yake kuwa ndio washukiwa wa ugaidi waliotekeleza mauaji jana kwenye ofisi za jarida maarufu la masuala ya utani la nchini Ufaransa, Charlie Hebdo. Msako mkali unaendelea kuwasaka.

Wametoa picha za watu hao, Cherif na Said Kouachi na kusema kuwa wana silaha na ni watu hatari.

_80126535_1b497c1e-6b7d-4baa-a989-e8f6c291d9d8

Mshukiwa wa tatu amejisalimisha mwenyewe.

Ufaransa imetangaza siku moja ya maombelezo kufuatia shambulio hilo lililosababisha vifo vya watu 12. Ulinzi mkali umeimarishwa nchini humo na wanajeshi wamesambazwa kulinda ofisi za vyombo vingine vya habari, makanisani, sehemu za usafiri na sehemu zingine muhimu.

Maandamano makubwa yamefanyika katika majiji mbalimbali duniani kuomboleza vifo vya watu hao huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa “Je suis Charlie” (I am Charlie).

Waandishi wanane akiwemo mhariri wa jarida hilo wameuwa pamoja na polisi wawili, fundi na mgeni aliyekuwa ametembelea ofisi hizo.

_80118073_5victims624_afp
Miongoni mwa waliouawa ni mwandishi wa masuala ya uchumi Bernard Maris, wachoraji maarufu wa katuni Wolinski na Cabu, Mhariri wa Charlie Hebdo, Stephane Charbonnier na mchoraji mwingine wa katuni Bernard Verlhac

Jarida hilo liliwaudhi baadhi ya waislamu siku zilizopita kwa kuchapisha katuni ya Mtume Muhammad. Watu hao walisikika wakitamka ‘Tumemlipizia Mtume Muhammad’ na ‘Allahu Akbar’

Chanzo: BBC News

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents