Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Godzilla amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano majira ya saa 10 alfajiri nyumbani kwao salasala jijini Dar Es Salaam.
Dada wa marehemu, Joyce Mbunda akiongea na Bongo5 amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema Godzilla alikuwa anasumbuliwa na tumbo.
Mwili wa Godzilla kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar Es Salaam.