Mitindo

Millen Magese afafanua kuhusu support anayoipata Tanzania kwenye kampeni ya Endometriosis

Jumapili hii Miss Tanzania wa zamani, mwanamitindo wa kimataifa na mshindi wa tuzo za BET, Millen Magese alidokeza kuhusu support anayoipata Tanzania kwenye kampeni yake dhidi ya ugonjwa wa Endometriosis.

b992a0d2-ae85-430a-aec7-177714051981
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania aishiye Afrika Kusini, Daxx (Kulia) alijitokeza kumuunga mkono Millen kwenye matembezi maalum kuhusu ugonjwa wa Endometriosis

Ilianza baada ya mlimbwende mwenzake, Miriam Odemba kumpongeza na kumshauri afanye pia matembezi ya uhamasishaji wa tatizo hilo nchini Tanzania. Millen alidai kuwa asingeweza kufanya hivyo kwa sasa kwakuwa support anayopata hususan kwenye tasnia ya urembo si kubwa na hivyo atafanya semina pekee ili kukuza kwanza uelewa wa tatizo lenyewe.

Millen ambaye mwaka huu ametunikiwa tuzo ya Umalkia wa Nguvu na Clouds Media Group, amedai kuwa wengi wametafsiri tofauti kauli hiyo na ameongea exclusively na Bongo5 akiwa Afrika Kusini kufafanua zaidi.

“Kwa mimi naamini kutoa ni moyo na sio utajiri. Kutaka kumsaidia mtu lazima inatoka kwenye moyo sio kulazimishwa, niliweke hilo sawa kwanza. Na huwa natoa shukrani kwa wale wote wachache wanaojitokeza kuendelea kunisaidia kila siku. Kwasababu sio rahisi kusaidia unajua hasa kwenye hili suala la Endometriosis. Mtu lazima aelewe ni kitu gani ambacho unakifanya ili aweze kukusaidia,” amesema.

Millen amedai alikuja nchini na kuendesha semina kuhusu tatizo hilo na amekiri kuwa licha ya kuwepo watu au taasisi zilizomsaidia, ni ngumu kupewa msaada kwa Tanzania.

“It’s hard to get support in Tanzania hasa hasa kwenye sekta yetu ya uanamitindo. Sisi tuko wachache sana na hawa wachache tuliopo huwa tunasaidiana sana. Watu wengi wanaonisupport mimi ni wanamuziki, waigizaji, waandishi wa habari, all the media houses wamekuwa mstari wa mbele kunisaidia, hata Clouds Media, followers wangu, my fans are so supportive, wazazi na wananchi wenzangu, nawathamini sana kwa kweli na wamefanya kazi kubwa. Sisi kama wenyewe tukiendelea kusaidiana zaidi hata tutaimarisha watu wengine. Sisi wenyewe tusimame, tusaidiane, tushirikishane katika mambo yote ambayo especially mambo ambayo yanasaidia jamii na tukiendelea kufanya hivyo watu wengi wataendelea kutusaidia. Hii ilikuwa ni safari ndefu sana, tusisubiri kwamba tukishatambuliwa na nchi zingine ndio pale tunapoanza kukumbushana kwamba we are proud,” amesisitiza.

60a33b3b-3f94-44f8-ac6a-faecf2ecb71e
Supermodels kutoka nchi mbalimbali walimuunga mkono Millen

Mrembo huyo tayari ameshafanya matembezi ya kampeni mpya ya tatizo hilo inayosisitiza kupatikana kwa tiba katika nchi za Nigeria na hivi wikiendi iliyomalizika nchini Afrika Kusini. Hata hivyo amesema ni ngumu kufanya matembezi hayo kwa Tanzania kwasababu watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusiana na Endometriosis.

“Hata sasa hivi wakitembea, watatembea kwasababu wamemuona mtanzania mwenzao anaumwa lakini itakuwa vizuri sana watu watasema kwamba we are supporting Millen kwamba anaumwa lakini tunaelewa anaumwa nini na hautamsaidia tu Millen bali jamii nzima. Nia yangu ni nzuri kabisa kwamba tunakuja tunaelimisha kwanza na nitatembea na madaktari kama nilivyofanya mwaka jana. Ilikuwa ngumu kuwaelimisha watu hata jina lenyewe kulitamka ni gumu.”

ee630ab0-abd1-4dac-b906-cff7b2a8a0b9

Amedai kuwa awamu hii atakuja kuanzia na semina kwenye shule za sekondari. Amesema anaamini kama akiendelea kuungwa mkono kwenye kampeni hiyo hata serikali itabaini ukubwa wa tatizo hilo na kushiriki kikamilifu kwakuwa tatizo hilo linaweza kuzuiliwa katika hatua zake za mwanzo.

10387793_944291489025723_1238061047_n
Miriam Odemba akionesha love kwa Millen

Kwa upande mwingine Millen ambaye tayari amefanyiwa upasuaji mara 13 kutokana na tatizo hilo na hivi karibuni alizidiwa na kulazwa, ameeleza sababu inayomfanya aendelee kuinuka tena na kuendelea na kampeni hiyo bila kuchoka wala kukata tamaa.

“Ninaamini kila mtu ana matatizo,” anasema Millen.

“Ukiyachukulia matatizo yako kuwa ni makubwa kuliko mwingine hilo linaweza kuwa tatizo kwasababu utakaa ndani utadhani kuwa ni wewe peke yako mwenye tatizo hilo. Kwangu mimi nimekaa na hili suala kwa miaka 23 mpaka naamua kuongea hili suala mwaka jana. Mimi kwanza nina familia yangu, wadogo zangu wananiangalia lakini kwa sasa nina zaidi ya familia, wasichana wadogo wananiangalia. Ninajitahidi kuwaonesha kwamba chochote unachoumwa, tambua kuwa haupo peke yako. Na mimi kuwa nje kujaribu kuwa hai inanifanya nijisikie vizuri sababu inanifanya niwe hai tena. Nikiwa hivyo watu wanaoniangalia nao wanakuwa hivyo pia.”

Millen amewaomba wanawake kushirikiana katika masuala mbalimbali na amewashukuru watanzania kwa jinsi wanavyomuunga mkono. “Naamini hili litamaliza chochote kilichotokea jana na nawashukuru tena watanzania, nitakuja nyumbani hivi karibuni.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents