Habari

Miriam Odemba asimulia alivyopambana hadi akakutana na Kanye West

Mwanamitindo wa kimataifa, Miriam Odemba amefunguka na kueleza jinsi alivyopambana katika majukwaa mbalimbali ya fashion ya kimaitafa na kufanikiwa kukonga mioyo ya mastaa mbalimbali wa kimataifa akiwemo rapa Kanye West wa Marekani.

miriamKanye
Miriam akicheza na Kanye West

Akizungumza katika kipindi cha Mkasi cha East Africa Television, Miriam alisema kila alikuwa akipata nafasi ya kupanda jukwaani, alijituma kuhakikisha anateka hisia za wabunifu wakubwa.

“Nimejitahidi sana katika mambo yangu ya modelling as Miriam Odemba ili nionekane,” alisema. “So kama 2013 nilialikwa na Ed Kavishe na Rose Marry katika Fashion Week. Nikasema I will work out in this fashion show everybody to know my name and understand what it is?” aliongeza.

“Nilifight Ed Kavishe akanipa invitation kwenda kwenye private party, nilivyoenda kwenye hiyo private party kulikuwa kuna all models. Nikasema this is my chance to show what it is and how is Miriam Odemba? Niliingia pale kama Twiga vile akikaa barabarani. Nikajiweka safi nasikia Kanye West anakuja hapa, nikasema nitamkomesha Kanye Wast hata kama kuna mabodygurd wake nitawaweka pembeni lazima anione na nitacheza naye.”

“Hata kama ukiwa na meneja kama kile kitu haujakidhamiria ni sawa na bure na kama hujakipenda you will never get ot. Nikasema hapa najiuza, nikaingia, Kanye West akaja nikasema nitaingia mpaka alipo tena hata VIP kwa sababu kulikuwa na matabaka. Naingia tu hivi nikaanza kucheza Kanye West mwenyewe alinifuata akacheza na mimi, nikasema mwenyezi Mungu asante ni kitu ambacho nilikuwa nakitaka,” alisema Miriam.

Pia Miriam ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike aliyezaa na raia wa Ufaransa, amesema kwa sasa bado anaishi Ufaransa pamoja na baba wa mtoto wake huku akiendelea na shughuli za modelling.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents