Habari

Mke wa billionea Msuya apandishwa kizimbani

Mke wa aliyekuwa bilionea wa madini maarufu jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Msuya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. akikabiliwa na mashtaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya.

p.txt

Mshtakiwa huyo akikabiliwa na mashtaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, alifikishwa mahakamani hapo jana asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi huku baadhi ya ndugu waliokuwa katika eneo la Mahakama wakilia kwa uchungu mkubwa. Miriam Msuya ambaye alisomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali Diana Lukondo, mbele ya Hakimu Mkazi, Magreth Bankika.

Naye Wakili Diana alidai kuwa, Mei 25, mwaka huu katika eneo la Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Aneth Msuya ambaye ni wifi yake. Wakati huo mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu, na pia kisheria mashitaka yanayomkabili hayana dhamana. Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

ANETH
Marehemu Aneth Msuya enzi za uhai wake

Miriam alikamatwa wiki chache zilizopita nyumbani kwake Sakina mkoani Arusha na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yanayomkabili. Wakati bilionea Msuya aliuawa Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi 22 wakati akiwa karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA), Aneth aliuawa kwa kuchinjwa shingo akiwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa matukio yaliyokuwa yakiripotiwa Polisi tangu Erasto auawe, ndugu hao wamekuwa wakipatwa na matukio mfululizo likiwemo la dada yake, Antuja Msuya kumwagiwa dawa inayodaiwa kuwa ni sumu akiwa amelala chumbani, na Esther Msuya na mumewe Samuel Charles walinusurika kuuawa kwa kupigwa risasi wakiwa katika baa jijini Dar es Salaam.

Hakimu Bankika aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 6, mwaka huu itakapotajwa tena.

CHANZO: HABARI LEO

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents