HabariSiasa

Mkoa wa Pwani wajiandaa na Uchaguzi mwishoni mwa wiki hii

Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Elisante Msuya ameeleza ,maandalizi ya uchaguzi wa Wilaya katika nafasi mbalimbali yamekamilika, ambapo uchaguzi wa wilaya zote utafanyika Jumapili, Octoba 2 mwaka huu.

Aidha uchaguzi wa Jumuiya ya wazazi katika wilaya tatu Mkoani hapo unafanyika Septemba 30 mwaka huu ,kutokana na kuahirishwa kwa sababu zilizojitokeza ikiwemo baadhi ya wagombea kukata rufaa.

Akifafanua juu ya uchaguzi huo ,leo septemba 28 ,Msuya ambae pia ni Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani alieleza ,wamejiandaa na wameshapanga wasimamizi wa uchaguzi ambao watapewa mafunzo kabla ya siku ya uchaguzi ili wafuate mfumo wa kusimamia.

Alieleza ,mchakato wa kurudishwa majina ya wagombea umeenda vizuri kwa kufuata vigezo na wanachama wamefurahia mchakato mzima ulivyokuwa .

“Waone namna Chama kilivyojiwekea kanuni, taratibu zake na kuzifuata sio Kama vyama vingine vya siasa ambavyo tunashuhudia vikikumbatia viongozi wale wale kila kipindi na kutoana kwa mitutu”

“Lakini sisi kupeana vijiti ni kawaida na ndio siasa ,Tena tunapeana kwa amani “alisema Msuya.

Vilevile alielezea uchaguzi wa Jumuiya za  wilaya ulienda  vizuri Ila kulikuwa na dosari ndogondogo katika uchaguzi wa Jumuiya ya wazazi kwenye kata ya Kibaha Mjini,Rufiji , Mkuranga ambazo uchaguzi utafanyika septemba 30 ijumaa.

Wakati huo huo, Msuya alisema katika uchaguzi wa mkoa nafasi ya Mjumbe Halmashauri Kuu Taifa muda wa kuchukua fomu umeongezwa ambapo utakuwa kuanzia octoba 1 hadi 5 mwaka huu.

Kwa upande wake, Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibitiz Muhidini Zakaria alitoa wito kwa wanachama wote wenye sifa za kushiriki uchaguzi kujiandaa kwa ajili ya kuwachagua viongozi bora na wajiepushe na rushwa.

‘Hii ni nafasi nyingine kwa wanachama wa CCM kushiriki kuchagua viongozi wao watakaoongoza miaka mitano, Kila kitu kiko tayari.

Zakaria aliwakumbusha wagombea umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu ili kuepuka malalamiko mara baada ya uchunguzi. ‘

Ni vyema wanachama wetu wote – wagombea pamoja na watakaoshiriki kwenye uchaguzi kuzingati taratibu na sheria za chama kwani sisi chama chetu kimejengwa kwa umoja na kufuata tarati

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents