MLAB yauwashia moto mtandao wa Waptrick


Studio ya Mlab ya jijini Dar es Salaam imelaani kitendo kinachofanywa na mtandao wa ‘waptrick.com’ kwa kusambaza nyimbo za wasanii wa Tanzania na kwingineko duniani bila kupewa ruhusu na wamiliki wa kazi hizo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook umesema mtandao huo haujawahi kuwasiliana na wamiliki wa kazi hizo kwa ajili ya kupewa ruhusa ya kusambaza nyimbo hizo bure.
“Tunasikitika kuwa site hii: http://www.waptrick.com/ imekuwa ikisambaza nyimbo za wasanii wetu wa kitanzania na tuna mashaka na walipoitoa ruhusa..hatutapenda kuwasemea wengine walioathirika ila kwa upande wetu hatujaingia mkataba nao wa kufanya mkataba wa mauzo ama kusambaza bure kazi zetu..hii inatutia shaka na kuhisi hata wasanii wengine waliopo kwenye list hiyo ni wazi wapo kwenye mlolongo huu.
Kwa kuwa mtandao huu bado kwanza hatujaufahamu kama unamilikiwa na watu wa ndani ama w anje ya nchi, tumeanza kufuatilia ila bila shaka lazima kuna connection ya mtu wa hapa nchini anaefanya mchezo huo mchafu. Tukiwa tunaendelea na juhudi za makusudi kutafuta wamiliki wa site hii pamoja na kuchunguza ni nani anaeratibu upasishaji wa hakimiliki za watu. Tunawaomba wapenzi na mashabiki wa M lab na mashabiki wa music wa Tanzania wasambaze habari hizi na wakemee mchezo huu mchafu, tunaomba pia blogs, na website zinazosaidia sana kusukuma music wetu hii zisambaze habari hi kwa mashabiki wa music wa Tanzania kususia website hii kama njia moja wapo ya kuokoa udhalilishwaji wa wasanii wetu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents