Habari

Mlima wa dhahabu uliogunduliwa na wanakijiji DR Congo, asilimia 90 ni dhahabu (+Video)

Serikali ya DR Congo ililazimika kutuma maafisa wa polisi kuimarisha usalama katika eneo ambalo kanda moja ya video iliwaonyesha wanakijiji wakichimba dhahabu kwa wingi.

Mwandishi wa BBC nchini DR Congo Byobe Malenga anasema kwamba Mlima huo upo kilomita 35 Kaskazini mwa eneo la Bukavu ndani ya mji mkuu wa mkoa wa Kusini mwa Kivu.

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPA

Habari za hivi karibuni zinasema kwamba serikali ililazimika kutuma maafisa wa polisi ili kuweka amani na kuchukua dhahabu ambayo wanaviji hao walikuwa wakichimba kwa wingi.

Taifa la DR Congo lina utajiri wa madini ikiwemo dhahabu na mlima uliokuwepo ndani ya video hiyo ni eneo lililosajiliwa ambapo lina wafanyakazi wake.

Inadaiwa asilimia 90 ya Mlima huo umejaa dhahabu. Klip hiyo fupi ya video inawaonyesha wanakijiji wakijikusanyia dhahabu juu ya Mlima huo na kwenda nazo nyumbani, huku wengine wakionekana kuziosha hapo hapo vipande hivyo vya dhahabu.

Mzozo wa dhahabu DR Congo

Shirika la Human Rights Watch linasema kwamba dhahabu ndio raslimali kubwa inayotegemewa na taifa hilo lakini kwasababu ni watu wachache wanaojinufaisha na madini hayo raia wengi wanasema hakuna usawa.

Hali hiyo imesababisha ujio wa makundi ya wapiganaji ambayo yamekuwa yakizozana na kusababisha maafa makubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents