Habari

Mo Dewji awajaza madini vijana kuelekea mwaka 2018

Mtanzania mfanyabiashara maarufu na Rais wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (MO) ametoa ujumbe kuelekea mwaka 2018 na kuwataka vijana na Watanzania kiujumla kuacha kulalamika mwaka 2018.

Dewji  amewasihi Watanzania kama wanaona hawapendezwi na kitu fulani njia nzuri ni kukibadili kitu hicho na kuacha kulalamika kwani hakutaweza kubadili jambo lolote lile.

“Kama hupendi kitu fulani, (jaribu) kibadilishe! Unataka kupunguza uzito? Badilisha milo yako, fanya mazoezi. Unataka kukutana na watu wapya? Toka nje, tembea na jichanganye na watu wengine! Kumbuka kulalamika hakubadilishi jambo usilolipenda!” aliandika Mo Dewji mtandaoni.

Mapema mwaka huu mfanyabishara huyo kijana aliibuka mshindi wa tuzo ya mtu aliyefanya vizuri katika Uongozi kwa Mwaka 2016 inayotolewa na Jarida la African Leadership.

Dewji alitunukiwa rasmi tuzo hiyo katika sherehe itakayofanyika Februari 24, mwaka huu katika Hoteli ya Southern Sun mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents