Michezo

Mo Dewji kwa uchungu awataja FCC

Muwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Mohammed Dewji amedai kuwa anasikitika kwamba wanafanya vikao na FCC na kukubaliana kumaliza halafu wanapata barua za kuanza upya.

Mo ameandika hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter ”Nasikitika kwamba tunafanya vikao na FCC na kukubaliana kumaliza halafu tunapata barua za kuanza upya. Labda Wabunge wapo sahihi kwamba kuna njama za kutukwamisha. Hii mbaya sana. Mipango yetu mikubwa inacheleweshwa.”- Mo Dewji

Klabu ya Simba kwa sasa ipo katika mchakato wa mabadiliko ya undeshaji na kwa muda mrefu mchakato huo umeonekana kukwama kwenye Tume ya Ushindani (FCC).

Tarehe 18 Novemba 2020 FCC iliwahi kutoka hadharani na kusema kuwa kuna baadhi ya taratibu hazikufuatwa na kusema kuwa ucheleweshwaji wa mchakato (transformation) wa kubadili mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba unatokana na mwitikio hafifu wa kampuni ya Simba Sports Club Company Limited wa kuwasilisha taarifa kamilifu na kwa wakati mbele ya Tume katika kufanikisha uchunguzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents