Michezo

Mohamed Issa aitwa Zanzibar Heroes

Kocha mkuu wa timu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman ametangaza kikosi chenye jumla ya wachezaji 30 watakao jiandaa na mashindano ya CECAFA Challange Cup yanayotarajiwa kufanyika nchini Kenya.

Kiungo wa kutumainiwa wa Mtibwa Sugar Mohamed Issa “Mo Banka” ameitwa katika kikosi cha timu ya Zanzibar kitakachoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi November 25 hadi Disember, mwaka 2017.

Mohamed Issa amekuwa na msimu mzuri mwaka huu baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na huku juzi akiitwa katika kikosi hicho cha Zanzibar Heroes.

Mtibwa waibamiza MONACO 5-0

Kikosi cha Mtibwa Sugar kinachodhaminiwa na watengenezaji wa trailler bora zilizothibitishwa na ISO Superdoll  baada ya mchezo  wa ligi kuu walielekea mkoani Lindi Jumapili na  kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Monaco FC yenye makazi yake Lideko mkoani humo ambapo wana tam tam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-0.

Magoli ya Mtibwa Sugar yakifungwa na Henry Joseph Shindika aliyefunga mawili, Kelvin Sabato, Riphat Khamis na Saleh Khamis Abdallah.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents