Burudani

Msafiri wa Kwetu Studios akanusha kusaini na Wanene Entertainment

Muongozaji wa video za Bongo anayefanya vizuri, Msafiri Shabani kutoka kampuni ya Kwetu Studio, amefafanua juu ya tetesi zilizoenea juu ya kusaini mkataba na kampuni ya Wanene kuchukua nafasi ya Hanscana.

Msafiri

Muongozaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hawezi kufanya kazi na kampuni ya Wanene kwa kuwa na yeye anamiliki kampuni yake.

“Hizo ni story tu sijafanya kazi na Wanene, sijawahi kufanya kazi na Wanene na sifanyi nao kazi kwa sababu mimi nina kampuni yangu inajitegemea,” amesema Msafiri.

“Sijasaini mkataba kwamba nafanya kazi na Wanene na wala Wanene hawajasaini na mimi,” ameongeza.

Msafiri ni mmoja kati ya waongozaji wenye uwezo mkubwa kwa sasa ndani ya Bongo ambao video anazotengeneza zinafanya vizuri kwenye TV tofauti tofauti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents