Burudani

Msanii hawezi kushindana na producer – Mr. T Touch

Producer kutoka Touch Sound, Mr. T Touch amesema ni vigumu kwa msanii kushindana na producer.

Kutokana na hilo Mr. T Touch amesema hawezi kushindana vita ambayo anajua atashinda.

“Wale ni wasanii wanaenda wanaonekana mbele ya macho ya watu wengi kuliko sisi ma-producer, watu wengine wameanza kuona sura ya T Touch hivi karibuni lakini kila kitu kinaenda kwa wakati,” amesema.

“Lakini ukisema kwamba tushindane, msanii hawezi kushindana na producer, mimi naweza kutoa ngoma za wasanii watatu kwa mpigo na zika-hit zote lakini msanii unapotoa wimbo unategemea utashindana na producer,” Touch ameiambia Bongo5.

Kauli ya Mr. T Touch inakuja mara baada kumchukua aliyekuwa msanii wa Nay wa Mitego, B Gway kutoka Free Nation ambapo awali alikuwa akifanya kazi Mr. T Touch. B Gway anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Na Stay.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents