Burudani

Msanii wa Nigeria YCEE azitaja nyimbo za Bongo Fleva zinazofanya vizuri kwao

Msanii wa Nigeria, Oludemilade Martin Alejo aka YCEE ambaye yupo nchini kwenye ziara yake ya muda mfupi amezitaja nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva ambazo kwa sasa zinachezwa zaidi nchini kwao.

Ycee 2

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio kuwa wimbo wa Kidogo wa Diamond aliowashirikisha P-Square umekuwa ukichezwa zaidi kwenye vituo vya radio na runinga za nchini humo inawezekana ikawa ni kila baada ya dakika 20.

Ycee pia ameongeza kuwa hata wimbo wa ‘Unconditionally Bae’ wa Sauti Soul waliomshirikisha Alikiba umekuwa ukichezwa mara nyingi pia kwenye vyombo hivyo. Pia ameutaja wimbo wa Vanessa Mdee, Niroge kufanya vizuri.

Msanii huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Omo Alhaji’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents