Habari

Mtangazaji wa BBC Swahili Abdul Mohamed adai tuzo za waandishi wa habari wa Afrika za CNN hazitilii maanani kazi za Kiswahili

Jana majina ya waandishi wa habari waliochaguliwa kuingia kwenye fainali ya ‘CNN Multichoice African Journalist Of The Year 2013’ yalitangazwa lakini hakuna mwandishi wa Tanzania aliyechaguliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho licha ya kuwepo waliotuma kazi zao akiwemo mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya BBC, Abdul Mohamed ambaye aliwahi kuwa mtangazaji wa Clouds TV.

BMwUFQmCQAIBzKV
Abdul (kushoto) akiwa na AY jijini London

Wakati yupo Clouds TV, Abdul alikuwa mtayarishaji mkuu na mtangazaji wa kipindi cha Sports Bar na kazi aliyoiwakilisha kwenye shindano hilo nii hapo chini ambapo alimpa Jacqueline Kombe kusoam kusoma script.

Akizungumzia kukosekana kwa mwandishi wa Tanzania kwenye fainali za shindano hilo, Abdul amesema:

“Nadhani tatizo sio waandishi wa Tanzania,waandaaji, hawatilii maanani kazi za wanaozungumza Kiswahili. Ukitaka kuamini, tusubiri uone kazi za hao walioingia fainali. Kuna umuhimu wa kuweka kipengele cha lugha ya Kiswahili kwenye hizo tuzo, tuone kama wakenya watawashinda watanzania kwenye ubora wa story.”

Unakubaliana na Abdul?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents