Uncategorized

Mtanzania ateuliwa na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis kuwa balozi wake nchini New Zealand

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amemteua Askofu Novatus Rugambwa mzaliwa wa Parokia ya Ishwandimi, Bukoba vijijini, Jimbo katoliki la Bukoba kuwa balozi wa Papa nchini New Zealand.

Askofu Novatus Rugambwa

Awali Askofu Novatus Rugambwa alikuwa balozi wa Papa Francis nchini Honduras.

Askofu Rugambwa ni moja ya Watanzania wakatoliki ambao wamewahi kupata cheo kikubwa cha uongozi katika kanisa katoliki, Baada ya Kardinali Laurean Rugambwa, Kardinali Pengo, na Askofu Protace Rugambwa mkuu wa uinjilishaji ulimwenguni na mshauri wa Papa huko Vatican.

Chanzo: https://www.dailynews.co.tz/news/2019-03-315ca04b2d205bf.aspx

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents