Habari

Mtoto wa Dereva aligongesha gari ya RC Mara,Baba na mama wazimia baada ya kupata taarifa hii

Mtoto wa Dereva aligongesha gari ya RC Mara,Baba na mama wazimia baada ya kupata taarifa hii

Gari ya mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima limepata ajali mbaya iliyosababishwa na mtoto wa dereva wake kuliiba na kutokomea nayo. Kadhalika deveva wa mkuu wa mkoa huyo pamoja na mkewe wamezimia baada ya kusikia tukio hilo la ajali.

Akizungumzia na Opera News kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki, alisema tukio hilo limetokeo leo dereva baada ya kuosha gari alifika nyumbani hakulizima kwa kuwa alikuwa anatoka kumfuata mkuu wa mkoa.

Alisema alivyoingia ndani dereva huyo alipata mgeni na kuzungumza naye.

“Wakati anazungumza na mgeni huyo mtoto wake wa miaka 24 alilichukua gari hilo bila ruhusa ya baba yake na walivyofika eneo la kanisani likamshinda na kuingia mtaroni. Hii ajali ni ya kizembe huyu kijana alikuwa spidi kubwa,” alisema. Kamanda alisema madhara ni makubwa katika ajali hiyo kwani utengenezaji wake sio chini ya Sh milioni 80.

Aidha, alisema kijana huyo ameumia na amepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu. “Baba yake alipokuja katika tukio la ajali alizimia na mkewe alivyopata hizo taarifa amezimia na wote wamepelekwa hospitali,” alisema Kamanda.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents