Burudani

Muziki gani utaitoa Tanzania kimataifa?, Wakazi, Fid Q, Zavara, Nchakalih na wengine wajadili

Jana kupitia akaunti yetu ya Twitter tulichokoza mjadala mrefu kwa kutweet: Nyimbo za Vanessa Mdee na MauaSama zimeprove kuwa watanzania wako tyr kulishwa nyimbo zenye ladha za kimataifa na wakatoa support.

world-music-icon

Ili muziki wa vijana wa Tanzania upate airtime kwenye international media hatuna budi kusupport wengine wenye muelekeo huo.

Wasikatishwe tamaa na zile kauli ‘wewe unaimba kimbele sana watanzania hawatakuelewa’ watanzania si washamba, tumeendelea na tunaelewa.

Tweets hizo zilivutia mjadala mrefu uliowahusisha wadau mbalimbali wa muziki wakiwemo rapper Fid Q, Wakazi, Zavara, Reuben Ndege aka Nchakalih na wengine uliokuwa hivi:

Conscious: Napenda kuona sasa kuna watu waliothubutu kufanya mziki wa kimataifa. Kazi nzuri kwenu. Swali linakuja, kwani watanzania waliwezaje kuwaelewa wadhungu mpaka washindwe kuwaelewa wakwao? #verryFUNNY.

Nchahkalih: Hapa waTZ wanaozungumziwa ni hawa wa Mjini au wa Vijijini? Na ‘kufika popote’ kipimo chake huwa nini?? Kupanda chati, shows au? Walio mjini na walio pata elimu wanazielewa sana hizo nyimbo..cha ajabu ni kwenye utafiti, Bongo flava ni #1. Kwa muda wangu mfupi kwenye media nimegundua Msanii akiwa REAL kwenye uimbaji wake…walengwa wake watamuelewa tu..iko wazi.

Kwa muda wangu mfupi kwenye media nimegundua Msanii akiwa REAL kwenye uimbaji wake.walengwa wake watamuelewa tu. Kwa ngoma kama ya vee money, kwa ninavyo ona, amefanya kitu REAL kwake…angejaribu kupiga zouk, matokeo sijui yangekuaje…

Wakazi: Ncha Kiingereza ingawa ni cha wakoloni, lakini tumeanza kujifunza toka darasa la tatu. Kwanini msanii asieleweke?

Tanzania watu hawapewi nafasi kiusawa, na kilichozoeleka ndo kitaendelea kutesa. nafasi ipo ya ku embrace all. Nigeria, Kuna ma Star wanaimba Kilugha, Ma Star wanaimba Pidgin English, na Ma Star wanaimba English.. ALL EQUAL

Fid: Wabongo hawasomeki.. Mbongo mwenzao ukimwaga ung’eng’e wanajifanya hawakuelewi halafu wanashabikia psquare. Mnakumbuka ile ‘mama don’t make me fall in laaavu’ ya Dibaji?Angeimba Mbongo angeambiwa hajui English.

NchaKalih: Hivi ile ya Dbanj sio PIDGIN ENGLISH?? English mboff mboff??

Fid: Whatever it is.. angeimba Mbongo angeambiwa anajifosi

Josue Murunga: Tatizo hmna “kiingereza cha kibongo”.Nameless,DJ cleo akiimba English ya kiKenya/SA its comfortable.

NchaKalih: Tatizo hmna “kiingereza cha kibongo.” Kama nimekuelewa hivi

Fid: Kiingereza cha kibongo kipo kwa akina Sir Nature na inspektah.. SMOOSI = SMOOTH.Na pia tusisahau NAVIO na KEKO hawatumii English ya kiganda.

Sapeur Josue Murunga: Lakini hatuongei hivyo kila siku.Ukikutana na Nameless,Femi Kuti or D’banj ataongea hivyo anavyoimba. True ,Navio ni wana be sana,ila Keko ni mfano kama Asa au Estelle ambao kipaji kinaforce umsikilize.

Adil Fauz [A-zee]: Wanashabikia midundo tu na melody nafkiri! maana sijaona watu wa hiphop wanaoshabikiwa kutoka naija.

Fid: Historically, Tz ndio home of pan africanism,nadhani ndio maana hatuna kiingereza cha Kibongo.

Sapeur Josue Murunga: I think KISWAHILI’s enough,don’t need English to be successful in Music,We Need irresistible Material.

Fid: Kilichobaki ndugu wasanii ni kukomaa ili kujikita rasmi kwenye ‘U-inter locally national’

RAWDGERS: The Kiswahili (in this world) is NOT enough, if we plan to influence our language internationally, we’ll have to use THEIR language.

Adil Fauz [A-zee]: Mi naona lugha sio ishu, maana huwa namsikiliza @sarkodie anavyo Rap anachengua lakini sielewi maana.

RAWDGERS: IRRESISTABLE material used to represent our IDENTITIY & express our SWAHILI culture.

TheHaissam: ‘english’ ‘swahili’ is just a language what’z the problem?

Zavara: Hizo ni harakati nnazoziunga mkono. Wanafanya kazi nzuri, kiswahili ni madini pekee yalobakia Bongo.Ni muhimu sana kuendeleza kiswahili. Naunga mkono sana harakati zote za uendelezaji wa lugha yetu adhimu. Pia kwenye hilo hilo watu ambao wana uwezo mzuri wa kiingereza na lugha nyingine naona ni vyema watumie tu.

Mtu kama Wakazi ye’ yuko vizuri zaidi kwenye kikoloni, na ana nafasi nzuri ughaibuni. Nnampongeza sana yeye. Nna tatizo sana na wale wanaojibaraguza na kikoloni na hawakiwezi na wakati huo huo Kiswa wanakizingua. Wako wengi sana wanatia aibu kujaribu kwa nguvu kikoloni na wanakosea hadi natakaga kijificha nkiwaskia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents