Habari

Mwalimu mkuu awakata nywele wanafunzi siku ya kufungua shule

Video ya mwalimu mkuu wa shule moja Zimbabwe akiwakata nywele wanafunzi kwa sababu walikuwa na mitindo ambayo ilikuwa kinyume na sheria za shule.

Mwalimu Mkuu Masimba Mupavaenda alisema Shule ya sekondari ya George Stark haiwezi kuvumilia “mitindo ya nywele ya namna ile.”

“Wanafunzi wana tabia ya kuja shuleni bila kujiandaa… kuna wengine wana nywele nzuri,lakini wengine wana mitindo ya kila aina ambayo haileti muonekano mzuri,” Bw Mupavaenda alisema.

Video hiyo yenye urefu wa zaidi ya dakika mbili inamuonesha mwalimu mkuu akiwakata nywele wanafunzi kwa mkasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents