HabariMichezo

Muamuzi aliyeipa Yanga penati afikishwa kwa pilato

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 4, 2022 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kuamua Mwamuzi wa kati, Florentina Zabron kumpeleka katika Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria 17 za mpira wa miguu katika mchezo tajwa hapo juu.

Kwa mujibu wa kamati ya (TPLB) Kamati ya Waamuzi ya TFF italitazama kitaalamu tukio la pigo la penati ya klabu ya Young Africans dhidi ya Geita Gold katika dakika ya 18 ya mchezo kabla ya kuishauri Kamati kwa kuzingatia kanuni ya 42:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti Waamuzi.

Tukio la Mwamuzi wa kati, Florentina Zabron kushindwa kutafsiri vema sheria 17 za mpira wa miguu limetokea kwenye mechi namba 74 Geita Gold FC 0-1 Young Africans SC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents