Burudani

Mwanamitindo wa Tanzania Niler Bernard apata shavu Afrika Kusini

Mwanamitindo kutoka Tanzania anayefanya vizuri kwa sasa, Niler Bernard anazidi kufanya vizuri katika kazi yake hasa baada ya kuongezewa dili kutoka kampuni ya Fullcircle, iliyopo Afrika Kusini.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo ameeleza kuwa amepata dili hilo baada ya kukaa kwa muda mrefu katika kitengo cha ‘development board’ na leo amepandishwa daraja jipya litakalo mpa fursa ya kufanya kazi kimataifa zaidi.

“Nilipofika mwaka jana mwezi wa tano ndiyo nikawa nimeingia kwenye ‘development board’ ambapo nikawa naendelezwa baada ya kunipokea wakawa wananitengeneza na kuangalia progress yangu, so nikawa nafanya kazi na kuwaza  lini nitaingia katika kwenye ‘ woman main board’. Basi  jana nilivyoenda kazini wakani-update kuingia kwenye ‘woman main board’, ambapo nitapata fursa wakija wateja kwenye website kutafuta models kwa ajili ya kazi zao watakuwa wananiona kwenye page za juu katika website hiyo,” amesema mrembo huyo.

Pia akaongeza kuwa “Kufanya kazi katika category hii ni fursa kwani sehemu hiyo wapo models wanaofanya kazi za International wakitokea nchi kama Brazil, Namibia, Ujerumani, Canada ila mimi ni Mtanzania pekee niliyopo kwenye cartegory hii hivyo ni kitu kikubwa na nina furaha kuwepo hapo.”

Mrembo huyo akasisitiza ” Kwa upande wa mkataba bado ni ule ule niliyoingia nao labda nifanye mabadiliko ndio nitaingia nao mkataba mpya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents