Burudani

Mwanamke wa Kichina maarufu kama ‘Malkia wa Pembe za Ndovu’ akamatwa nchini akisafirisha pembe zenye thamani ya £1.62m

Mwanamke wa China anayedaiwa kuongoza genge kubwa zaidi la usafirishaji pembe za ndovu barani Afrika amekamatwa nchini.

stream_img

Akipewa jina la utani “Ivory Queen”, Yang Feng Glan anadaiwa kusafirisha pembe za ndovu 706 kutoka nchini kwenda Mashariki ya mbali.

Glan, 66, anadaiwa kuwa na ukaribu na majangili wa Afrika Mashariki na walanguzi wa China. Anadaiwa pia kuyasaidia kifedha makundi ya majangili zinazoyasaidia kununua silaha na magari na pia kutoa rushwa ili kufanya kazi bila vikwazo.

Mama huyo alifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na anashtakiwa kwa kusafirisha pembe za ndovu zenye thamani ya paundi milioni 1.62 katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2014 ingawa wapelelezi wanaamini amekuwa akifanya kazi hiyo tangu miaka 1980.

Alifikishwa mahakamani akiwa na wanaume wawili raia wa Tanzania ambao wamekuwa wasaidizi wake wakuu. Anaendelea kushikiliwa na polisi.

Kukamatwa kwa mama huyo kumekuja baada ya kuwepo upelelezi wa mwaka mzima na kikosi cha kukabiliana na ujangili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents