Habari

Mwanasheria ataka wanawake wanaovaa jeans mchaniko ‘Ripped Jeans’ wabakwe

Mwanasheria maarufu nchini Misri,  Nabih al-Wahsh amesema wanawake wanaovaa nguo aina ya jinsi za kuchanika maarufu kwa jina la ‘Ripped Jeans’ wabakwe kwani wanajitakia wenyewe.

Mwanasheria, Nabih al-Wahsh

Bwana Nabil amesema wanawake wanaovaa jinsi au suruali kama hizo huwa wanakusudio la kuzalilishwa kijinsia iwe kwa kushikwa au hata kwa kubakwa kwani hakuna mwanaume wa misri ambaye angejizuia kuwaangalia wanavyopita karibu yake.

“Mwanamke kuvaa nguo iliyochanika kwenye mapaja ni dhahiri kuwa anawakariisha wanaume wamdhalilishe iwe kwa kumshika, kubaka au hata kingono na hilo ni jukumu la wanaume wa Misri hatuwezi kuvumilia tutafanya hivyo.“amesema Nabil al-Wahsh kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Al-Assema.

Mwanasheria huyo alitoa maoni hayo kwenye mahojiano maalumu katika kipindi hiki ambapo Misri inafanya mabadiliko ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Hata hivyo, Mwanasheria huyo ameongeza kusema kuwa “Wasichana wanatakiwa kwanza wajiheshimu ndipo ndipo waheshimiwe na wanaume. Tunapaswa kutambua kuwa kulinda utamaduni wetu ni jambo muhimu kuliko kulinda mipaka ya nchi.”

Hii sio mara ya kwanza kwa Mwanasheria huyo kutoa maoni yenye mkanganyiko akiwa mubashara kwenye vituo vya Tv, kwani mwaka jana alimpiga na kiatu kichwani Imam aliyesema kuvaa Hijab au Niqab sio lazima kwa mwanamke wa kiislamu.Tazama Mwanasheria huyo akifunguka kuhusu marekebisho hayo na waandishi wa habari

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents