Burudani

Mwasiti apanga kuachia ngoma ya Hip Hop

Mwasiti amesema Fid Q, Mwana FA pamoja na Godzilla wamemwambia wapo tayari kumwandikia wimbo wa Hip Hop ili na yeye aoneshe uwezo wake katika muziki huo.

Mwasiti

Muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV kuwa ana nia ya kubadili muziki wake kidogo ili kupata ladha nyingine.

“Mimi napenda Hip Hop sana, sema sijawahi kujaribu,” alisema.

“Nitajaribu kuachia wimbo kwa sababu nimepata bahati Mwana FA kasema ataniandikia, Fid Q amesema ataniandikia, Nick wa Pili pamoja na Godzilla wapo tayari kuniandikia. Sasa ni mimi tu nikamilishe halafu niseme lini itatoka,” aliongeza Mwasiti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents