Habari

Mwenge wa uhuru waja na neema

Mwenge wa Uhuru  umeanza kukimbizwa katika Mkoa wa Arusha ambapo utakapokuwepo Mkoani humo, utaweka mawe ya msingi,kuzindua, kufungua na kukagua miradi 53 ya maendeleo  yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 581.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amepokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere katika kijiji cha Kansay kilichopo Wilaya ya Karatu.

Mwenge wa Uhuru  umeanzia Wilaya ya Karatu kwa kupita katika miradi nane yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion 3.4. Miongoni mwa miradi hiyo ni wa Ujenzi wa maabara ya kisasa katika kituo cha afya cha Endabash, pamoja na mradi wa matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Tehama) .

Mwenge huo utakuwepo katika mkoa wa Arusha kwa siku sita, katika Wilaya sita na unatarajia kukimbizwa kwa jumla ya kilometa 950.35.

By – BAKARI WAZIRI

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents